Header Ads

ad

FAHAMU MAANA ZA VIBAO VYA NAMBA ZA MAGARI TANZANIA


Gari lolote linapoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi, ama binafsi au ya kibiashara, kabla halijaanza kufanya shughuli hiyo hutakiwa kusajiliwa ili lipatiwe vibali na kuweza kulipa tozo mbalimbali.

Kila gari linalosajiliwa, hupewa namba za utambulisho ambazo halitambulisha husika na hazifanani na gari jingine lolote.
Licha ya namba hizi kutambulisha magari, lakini wakati mwingine zinatumika kutambulisha makundi ya magari na mmiliki wake. Mfano wa utambulisho wa makundi ya magari ni yale yanayomilikiwa na serikali, magari ya biashara, magari ya balozi na mashirika ya kimataifa.

Namba za magari zionekanavyo leo, sivyo zilivyokuwa zikiandikwa katika miaka ya nyuma, zimekua zikibadilishwa mara kwa mara lengo likiwa ni kuleta urahisi katika usajili. Katika miaka ya 1980, namba za magari za Tanzania zilikuwa zikiandikwa, TXX 9999 (XX zinawakilisha herufi) wakati miaka ya 1990 zilikuwa zikiandikwa, XXX 9999.

Baada ya kuanza kwa Karne ya 21, mfumo wa namba za usajili wa magari nao ulibadilika na kuwa T 999 XXX ambapo pia walijumuisha bendera ya Tanzania katika vibao vya namba.
Hapa chini ni maelezo ya aina mbalimbali za namba za utambulisho wa magari;

1. Kibao cha gari cha rangi ya njano kilichoanza na herufi T

Kibao hiki kinaonyesha kuwa gari husika limesajiliwa kutumika kwa ajili ya shughuli binafsi pekee (private car). Magari yenye vibao hivi hayaruhusiwi kutumika kwa ajili ya biashara mfano kubeba abiria hata kama linauwezo wa kufanya hivyo.

2.  Kibao chenye rangi nyeupe na namba inayoanza na herufi T
Kibao hiki kinaonyesha kuwa, gari husika limesajiliwa kwa ajili ya matumizi ya biashara (commercial use). Mfano wa magari haya ni daladala za abiria na taxi. Gari zinazosajiliwa kwa namba hii sio lazima ziwe kubwa za kubeba abiria wengi, hata ukiwa na gari dogo, unaweza ukaamua kulisaili kama gari la biashara.

3. Kibao chenye rangi ya njano na namba haianzi na herufi T


Kibao hiki kinaonyesha kuwa, gari husika linamilikiwa na taasisi ya umma au serikali. Hapa kuna makundi yafuatayo:
(a) SU – Shirika la Umma, mfano vyuo vikuu vya serikali
(b) SM – Serikali za Mitaa, mfano ni halmashauri
(c) STK, STL, STJ – Serikali, mfano ni wizara

4. Kibao chenye rangi nyekundu na namba inayoanza na herufi DFP au DFPA

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika limetolewa kwa ajili ya matumizi ya miradi inayofadhiliwa na wafadhili mbalimbali kutoka nje ya nchi.

5. Kibao chenye rangi ya bluu na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na herufi CD kisha namba tena.
Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na moja ya shirika la umoja wa mataifa. Mfano shirika la Afya Duniani (WHO).

6. Kibao chenye rangi ya kijani na namba inayoanza na herufi T kufuatiwa na namba na kisha herufi CD kisha namba.
1

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na ofisi za ubalozi wa nchi fulani. Mfano ubalozi wa Ufaransa.
7. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeanza na PT. Namba hizi huwa za njano.


Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Polisi la Tanzania.
8. Kibao chenye rangi nyeusi na namba zimeandiwa kwa rangi nyeupe

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Wananchi (JW). Namba hizi huwa na herufi JW.
9. Kibao chenye rangi ya kijani na namba zenye herufi MT

Kibao hiki kinabeba maana kuwa gari husika linamilikiwa na Jeshi la Magereza la Tanzania.

10. Namba za magari zinazowawakilisha viongozi.
Namba hizi huwa na herufi za mwanzo ama za taasisi, idara, wizara au mamlaka ambayo kiongozi husika anafanyia kazi. Mfano hapa ni namba za magari ya Majaji, Mawaziri na Manaibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa n.k.

11. Namba za magari zenye majina watu


No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.