Beka Flavour achukizwa kushindanishwa na Aslay
Msanii Beka Flavour amesema hapendezwi jinsi baadhi ya watu na mitandao inavyomshindanisha na Aslay.
Beka ambaye alikuwa kundi moja (Yamoto Band) na Aslya, ameiambia E-Newz ya EATV kuwa yeye hafanyi muziki wa ushindani hivyo ni vyema watu wakasapoti kazi zao wote kwa pamoja pindi zinapotoka.
“Siku hizi hamna muziki wa maneno mengi na kiki sema mimi nilikuwa naona vile vitu vilikuwa vinaendelea mtandaoni. Ukweli hamna kitu kama hicho mimi nafanya muziki wangu binafsi halafu ninaamini ni wakwangu, mimi ndiyo Justine Beiber wa Bongo,” amesema na kuendelea.
“Wanatakiwa watusapoti, siyo poa wanavyoandika wanatushindanisha halafu mimi sifanyi muziki wa ushindani na miaka 100 siwezi nikafanya muziki wa ushindani sina tatizo na msanii yeyote kutoka Tanzania,” amesisitiza.
Beka Flavour kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Sikinai’, ikiwa ni baada ya kutikisa ipasavyo na ngoma ya Libebe.