Bifu la Diamond na Kiba Limeanza Upya...Huwa silagi Vipusa – Diamond
Bado mistari ya Diamond kupitia beat ya Fid Q ‘Fresh’ inaleta utata na kushindwa kueleweka ni nani haswa analengwa.
Kupitia mtandao wa Instagram Diamond ameweka audio clip yenye sekunde 25 akichana vilivyo. Hapa chini nimekuwekea kinachosikika katika clip hiyo.
Kufanya verse moja tu naona povu linawashuka, kina dada wavaa vi-top na vibukta/Hawatoi ngoma kazi twiter kunisuta, kusafiria nyota nawapa pia na jua ruksa/Wengine vishavu nukata, lips kama tuta, najiuliza ni nani au wameumbwa na hulka/Wapo pamoja post sina mafuta, msiniletee nuksi huwa silagi vipusa/
Huu ni muendelezo mashairi kutoka Diamond yasiyoeleweka nini maana yake baada ya kusika katika Fresh Remix (original) ambayo imeleta maneno mengi mitandaoni.