Msichana wa miaka 13 aliyebakwa aruhusiwa kutoa mimba India
Mahakama ya juu zaidi nchini India imempa ruhusa msichana mja mzito muathirwa wa ubakaji mwenye umri wa miaka 13 kutoka mji wa Mumbai kutoa mimba hiyo.
Msichana huyo mwenye uja uzito wa wiki 32 alikuw anataka ruhusa ya mahakama kutoa mimba hiyo kwa kuwa mahakama za India uruhusu mimba ya zaidi ya wiki 20 kutolewa ikiwa tu maisha ya mama yamo hatarini.
Mimba hiyo iligunduliwa wakati wazazi wake walimpeleka mtoto huyo kwa daktari kutafuta matibabu ya unene wa mwili.
Mimba hiyo inatarajiwa kutolea siku ya Ijumaa, kwa mujibu wa wakili wake
Msichana huyo anadaiwa kubakwa na rafiki wa babake ambaye kwa sasa amekamatwa.
Uamuzi wa kumruhusu msichana huyo kutoa mimba ulifanywa na jopo la majaji watatu ambao walitumia ripoti kutoka kwa madaktari kutoka hospitali ya JJ mjini Mumbai.
Keshi ya msichana hiyo inafanyika baada ya msichana mwingine wa umri wa miaka 10 ambaye ambaye naye alikuwa ni muathiriwa wa ubakaji, alijifungua mtoto msichana katika mji ulio Kaskazini wa Chandigarh.
Alikuwa na mimba ya wiki 32. Mahakama haikumrusu kutoa mimba mimba baada ya madaktari kusema kutolewa mimba hiyo kulikuwa hatari kwa maisha yake.
Mwezi Mei kisa kama hicho kiliripotiwa katika mji wa kaskazini wa Haryana ambapo msichana wa uamri wa miaka 10 ambaye alidaiwa kubakwa na babake wa kambo aliruhusiwa kutoa mimba.