Header Ads

ad

Serikali Yashangaa Tundu Lieu Kuchangiwa Mtandaoni yasema Inasubiri Ruhusa Ya Familia


Hayo yameelezwa leo Septemba 21 na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoni Tanga.
Waziri Mwalimu amesema serikali haijajitoa na haitafanya hivyo katika matibabu ya Mbunge huyo na kwamba imeshangazwa na taarifa za kuwataka wasamaria wema kuchangia matibabu ya Lissu.

"Naitaka familia ya Mhe Lissu na watanzania watambuae kuwa serikali ipo tayari kugharamia usafiri na matibabu hayo popote pale atakapopelekwa Duniani, Tundu Lissu siyo mtu wa kuchangiwa na wasamaria wema katika matibabu yake kama inavyoonekana na kujitokeza sasa” alisema Ummy.

Hatua hiyo imekuja wakati CHADEMA ikiendelea kuchangisha fedha kwa wadau mbalimbali na wasamaria wema kwa ajali ya kugharamia matibabu ya Mbunge huyo, ambapo kwa mujibu wa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa mpaka sasa gharama za matibabu zimeshafika milioni 150.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.