ORODHA YA MIKOA INAYOONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI
Mkoa wa Njombe umetajwa kuwa ndio mkoa unaaongoza zaidi katika maambukizi ya virusi vya UKIMWI na kuwa na watu wengi wanaoishi na virusi hivyo.
Takwimu zilizotolewa na Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) za mwaka 2011/2012 zinaonyesha kuwa Mkoa wa Njombe una maabukizi ya UKIMWI kwa 14.8% ambapo kati ya watu 100 takribani watu 15 wana maambukizi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI Tanzania (TACAIDS) Dk. Leonard Maboko ameyaeleza hayo na kuongeza kuwa mikoa inayofuatia ni Iringa pamoja na Mbeya ambapo kiwango cha maambukizi katika mikoa hiyo ni 9%.
“Mkoa wa Njombe una kiwango cha maambukizo kwa 14.8% ambayo ni katika watu 100 takriban 15 wana maabukizi ya virusi vya ukimwi na inafuatiwa na Mkoa wa Iringa pamoja na Mkoa wa Mbeya ambao kiwango cha maambukizo ni 9%. Yani katika kila watu 100, watu 9 wanaongoza kwa maambukizi ya UKIMWI,” amesema Dk. Leonard Maboko
.
Dk. Leonard aliutaja Mkoa wa Manyara kuwa ndio wenye kiwango kidogo kabisa cha maambukizi ambapo kiwango cha maabukizi ni 1.5% huku akieleza kuwa takwimu hizo zimejikita zaidi katika tofauti za kijiografia pamoja na tofauti za makundi
.
“Mkoa wa chini kabisa ni Manyara kutokana na takwimu hizo ambayo ni 1.5%, lakini bado hizi hazimaanishi kwamba Mkoa wa Manyara hakuna maeneo ambayo yana kiwango kikubwa,” Amesema.
Aidha Dk. Maboko ameeleza kuwa tume hiyo imetenga fedha maalumu kwa ajili ya kupambana na UKIMWI katika makundi mbalimbali kama vile wavuvi na maeneo ya machimbo.
“Tutakuwa na hela mbayo tutaitoa hivi karibuni kwa ajili ya maeneo ya wavuvi kama Lake Victoria.. kwa hiyo haya tunatoa kipaumbele kulingana na takwimu zinavyotuonyesha wapi tuelekeze nguvu,” amesema Dk. Maboko.
No comments: