Header Ads

ad

KATIBU WA CHADEMA AJIUNGA CCM


Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Simanjiro, Mkoa wa Manyara, Meshack Turento ametangaza kujivua wadhifa huo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi akidai chama hicho (CHADEMA) imewatelekeza.
Meshack Turento

Akizungumza jijini Arusha Turento alidai kuwa, kabla ya kujiunga na CHADEMA alikuwa mwanachana wa CCM, lakini baadae aliona chama hicho kimepoteza mwelekeo na kujiunga na CHADEMA, ila sasa ameamua kurejea CCM baada ya kuona ndani ya CCM kuna mabadiliko makubwa
.
Pia alisema kuwa ameridhishwa na utendaji kazi wa Rais Magufuli ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM taifa kwa kuimarisha chama hicho na kukijengea mfumo mzuri wa madaraka

Hata hivyo alikanusha taarifa za yeye kutishwa kukamatiwĂ  mifugo yake iwapo ataendelea kubaki CHADEMA na kudai si za kweli na wala hajanunuliwa.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.