Tamko la Jukwaa la Katiba Tanzania kuhusu Katiba Mpya
Jukwaa la Katiba Tanzania ‘JUKATA’ limewataka viongozi wa Serikali ya Tanzania, wajipime ni namna gani wanatekeleza ahadi walizozitoa kwa Watanzania ikiwemo suala la Katiba mpya.
Mkurugenzi Mtendaji wa JUKATA, Hebron Mwakagenda amesema baada ya kuifuatilia na kuichambua Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa miaka miwili mfululizo, wamebaini Serikali haijatenga fedha kwa ajili ya kukamilisha mchakato huo.
>>>”Kutokana na kutotengwa kwa fedha yoyote kwenye Bajeti ya Serikali kwa ajili ya mchakato huu adhimu, lakini chini ya utawala huu wa Awamu ya Tano yameanza kufifia.”
Kuhusu matukio yanayoendelea nchini, ikiwemo kuzuiwa kuonyeshwa Bunge LIVE na kuzuiwa mikutano ya siasa, Mwakagenda amesema ni matukio yanayotokana na udhaifu wa Katiba huku akisema JUKATA wanaungana na Watanzania wote kulaani jaribio la kumtoa uhai, Tundu Lissu.
Aidha, amesema kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika Kenya na kufutwa na Mahakama inaonyesha uimara wa Katiba ya Kenya, ambapo kuna umuhimu na mafunzo kwa Tanzania ili matokeo ya Rais kuhojiwa Mahakamani.
>>>”Kama ikitokea hakuna uwezekano wa kukamilisha mchakato wa Katiba kabla ya mwaka 2020, kutahitajika marekebisho ya msingi katika Katiba ya Tanzania ya mwaka 1977, Katiba ya Zanzibar 1984 ili kushughulikiwa kwenye uchaguzi.”
No comments: