Watu wafanya maandalizi ya mwisho kabla kuwasili kimbunga Irma
Visiwa vilivyo eneo la Caribbean vimefanya matayarisho ya mwisho kwa kimbunga Irma, ambacho ni kimbunga chenye nguvu zaidi kwa mwongo mmoja, huku maafisa wakionya kuwa kimbunga hicho kinaweza kuwa chenye madhara makubwa.
Kimbunga Irma cha kiwango cha tano kimepata nguvu ya upepo wa kasi ya hadi kilomita 295 kwa saa.
Kimbunga hicho kinatarajiwa kupiga visiwa vya Leeward kabla ya kuelekea huko Puerto Rico, Haiti na Floirda.
Watu wameamrishwa kuondoka kwa lazima eneo la magharibi mwa Florida.
Wageni watatakiwa kuondoka Jumatano asubuhi huku wenyeji nao wakitakiwa kunodoka ifikapo jioni na safari zote za ndege kusitishwa.
Viwanja vya ndege vimefungwa kwenye visiwa kadha, maeneo maarufu ya kustarehe na mamlaka zimewataka watu kuenda maeneo salama.
Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza hali ya tahadhari huko Florida, Puerto Rico ba visiwa vya Virgin na kutangaza mikakati ya kukabiliana na majanga sehemu hizo.