Header Ads

ad

Euro Million 400 Kumng'oa Messi Barcelona


Kuna wakati fulani hivi mwanamuziki mmoja aliimba ‘ mwenye pesa sio mwenzie ‘. Pesa ina jeuri yake hapa ulimwenguni.

Baada ya Paris Saint-Germaine kuibomoa FC Barcelona mwanzoni mwa msimu huu mpya wa ligi kuu nchini Uhispania ( La Liga ) kwa kumchukua Neymar Jr kwa uhamisho ulioweka rekodi ya dunia katika soka, Manchester City nao wapiga hodi Catalunya kuendelea
kuibomoa klabu hiyo kwa uhamisho ambao una thamani mara mbili zaidi ya wa Neymar Jr.

PSG walimnyakua Neymar Jr kwa Euro milioni 222 na sasa Manchester city wamemtengea Lionel Messi mchezaji bora wa dunia mara tano kitita cha Euro milioni 400 ili kumng’oa FC Barcelona na kuingia Etihad kwenye mikikimikiki ya ligi kuu nchini England.

Ni habari ya kushitua kwa wapenzi na wanachama wa miamba hiyo ya soka nchini Uhispania na inazidi kupata uhakika wake baada ya mchezaji huyo kugoma kuongeza mkataba wake wa kukaa Nou camp baada ya huu wa sasa kuelekea ukingoni. Mkataba wake na Barcelona unakwisha majira ya joto mwakani hali inayomfanya kuweza kuzungumza na klabu yoyote kuanzia mwezi januari mwakani.

Tayari Manchester city wameanza mazungumzo ya pembeni na watu wa karibu wa gwiji hilo la soka toka Argentina ambaye ameanza vyema msimu wa La Liga baada ya kutupia nyavuni mara 11 kitu ambacho kimeiwezesha FC Barcelona kutopoteza mchezo wowote mpaka sasa.

Baada ya kuondoka Neymar Jr, Barcelona walianza kampeni za kumnasa mshambuliaji mahiri wa Liverpool Phillipe Countinho lakini majogoo hao wa London waliwawekea ngumu licha ya mchezaji husika kuomba auzwe . Tayari vibopa wa PSG wameonesha nia pia ya kumnasa mshambuliaji huyo katika mwendelezo wa kuidhoofisha Barcelona kama walivyofanya kwa Neymar.

Barcelona wamepanga kumchukua Countinho mwezi januari lakini taarifa za chini kwa chini zinasema PSG wamepita mlango wa nyuma mchezaji huyo asiondoke Liverpool mwezi januari ili wao waweze kumchukua majira ya joto. Kutokana na masharti ya matumizi ya fedha kwa vilabu vya Ulaya, PSG hawawezi kuingia vitani na Barca mwezi januari baada ya kutumia kiwango kikubwa mwanzoni mwa msimu kwa manunuzi ya akina Neymar.

Hili litazidi kuivuruga Barcelona. Lakini pia Countinho ameichezea Liverpool kwenye michuano ya klabu hivyo ni ngumu kucheza katika timu mbili tofauti katika msimu mmoja kitu ambacho kinazidi kuwapa uhakika PSG uwepo wa mshambuliaji huyo Liverpool mpaka majira ya joto.

Raisi wa klabu hiyo bwana Josep Maria baada ya tetesi hizi kuwafikia alisema haoni sababu ya Messi kuondoka Catalunya sehemu ambayo ameijenga fani yake toka akiwa mdogo .
” nina imani kubwa ya kumsainisha mkataba mpya Lionel Messi utakaomuweka hapa klabuni mpaka mwaka 2021 kama ilivyotangazwa mapema . Hapa ni nyumbani kwake ” alisema Josep Maria akiongea na Opt

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.