Header Ads

ad

HAMISA MOBETO AMSHTAKI DIAMOND KWA KUMDHALILISHA


Mlimbwende na mwanamitindo Hamisa Mobeto amepeleka malalamiko yake katika Mahakama ya watoto na kutaka mzazi mwenzake ambaye ni msanii wa muziki Tanzania, Naseeb Abdul maarufu kama Diamond Platinumz aitwe kwa madai ya kushindwa kumuomba radhi na kutoa matunzo ya mtoto.

Wito huo kwa Diamond umewasilishwa na mawakili wa Mobetto, Abdullah Zulu na Walter Godluck kutoka Kampuni ya Uwakili ya Century Attorneys.
Katika wito huo Hamisa anadai kuwa dimond amemdhalilisha na ameshindwa kutoa matunzo ya mtoto kwa muda wa miezi miwili.

Wakili anayesimamia dai hilo la Hamisa Mobetto, Abdullah Zulu amesema kuwa mteja wake alimpelekea Diamond nitisi ya kumtaka amuombe radhi pamoja na kumpetia matumizi ya mtoto ndani ya siku saba.

“Baada ya kuona kimya tulipeleka kesi katika Mahakama ya Kisutu upande wa watoto (The Juvenile Court Of Dar es Salaam) na leo(Alhamisi) tumepewa barua ya wito na tayari mwanasheria wa mwanamuziki huyo ameipokea,” amesema Wakili Zulu.
Kesi hiyo itaanza kusikilizwa Oktona 30, mwaka huu.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.