Header Ads

ad

TAARIFA YA TRA KUHUSU PICHA ZA MAGARI YENYE NAMBA ZA USAJILI ZINAZOFANANA


Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetolea ufafanuzi picha zenye magari yenye namba zilizofanana yanayosambazwa mitandaoni na kueleza kuwa, picha hizo ni za siku nyingi na kwamba tayari matatizo hayo yamekwisha kutatuliwa.

TRA imelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya watu wengi kujiuliza maswali baada ya kuona picha hizo zinazoonyesha magari mawili yakiwa na namba za usaji zilizofanana, huku baadhi ya watu wakiitupia lawama mamlaka hiyo kuwa haiko makini kwenye utendaji kazi wake.

“Tunapenda kuwafahamisha wadau na wananchi wote kuwa, picha za magari zenye namba za usajili zinazofanana ambazo zinasambazwa mitandaoni, ni za siku nyingi na zilishafanyiwa kazi kikamilifu, na kubaini chanzo na wahusika,” wameeleza TRA katika taarifa yao.

Hapa chini ni baadhi ya picha ambazo zimekuwa zikisambazwa kwenye mitandao ya kijamii

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.