Header Ads

ad

Mmoja CHADEMA sawa na mia CCM



Mbunge wa Bunda Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Ester Bulaya amefunguka na kusema uwezo wa wabunge wa CHADEMA kwa wanawake ni mkubwa mno ukilinganisha na uwezo wa wabunge wanawake wa CCM na kusema Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa CCM.
Bulaya amesema hayo alipokuwa akihojiwa na kituo kimoja cha Televisheni nchini Kenya alipokwenda kumtembelea na kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye anapatiwa matibabu kufuatia kupigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017. 

"Tanzania wanawake wa upinzani tunauwezo zaidi kuliko wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kabisa, sisi tunamsemo wetu kwamba Mbunge mmoja wa CHADEMA ni sawa na wabunge 100 wa Chama Cha Mapinduzi na hiyo ni kauli ya Mwenyekiti wetu Freeman Mbowe, sasa ukiona wabunge wengine wageni Bungeni hawana uzoefu, wamekuja na wanataka kupata umaarufu anafanya vioja sisi wazoefu ambao tumepambana na kushindana na wakongwe wa kwenye chama hicho tunampuuza" alisema Ester Bulaya 

Mbali na hilo Ester Bulaya amesema amemkuta Mbunge Tundu Lissu akiwa anaendelea vyema na kusema amempa ujumbe kwa Watanzania kuwa wajiandae. 

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.