PICHA: LOWASSA AMTEMBELEA TUNDU LISSU HOSPITALI
Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa leo Oktoba 23 amemtembelea na kumjulia hali Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibu Nairobi nchini Kenya.
Katika safari hiyo, Lowassa alikuwa ameandamana na mke wake, Mama Reginal Lowassa na wameonekana kwenye picha wakiwa na furaha na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
No comments: