TUNDU LISSU ASABABISHA POLISI KUVAMIA MKUTANO WA SHEIKH PONDA
Jeshi la Polisi limevamia na kuzuia mkutano wa Sheikh Issa Ponda aliokuwa amepanga kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, mara baada ya kurejea kutoka Nairobi ambako alizungumza na Lissu.
Mkutano huo ulikuwa umeandaliwa kufanyika katika Hoteli ya Iris, iliyopo eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam jana asubuhi.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo ameeleza kwamba, baadhi ya waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye ukumbi huo wamekamatwa na polisi.
Sheikh Ponda alikwenda Nairobi kumjulia hali mbunge huyo anayepatiwa matibabu huko baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7 mwaka huu.
No comments: