Header Ads

ad

Walinzi wa kiongozi wauawa kwa kupigwa risasi


Walinzi wawili wa Mfalme wa Saudi Arabia wameuwawa kwa kupigwa risasi baada ya mtu mmoja kuvamia na kushambulia kasri hilo.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani imesema, mtu aliyetekeleza shambulio hilo aliendesha gari hadi kwenye lango kuu la kasri la Al Salaam kabla ya kuwafyatulia risasi walinzi waliokuwa lindoni
.
Mtu huyo ametambuliwa kwa jina la Mansour Al – Amri mwenye umri wa miaka 28 alishambulia kasri hilo jana Jumamosi saa tisa alasiri kwa saa za Saudia, lakini aliuwawa baada ye na walinzi.

Mapema kabla ya shambulio hilo Ubalozi wa Marekani nchini humo uliwaonya raia wake kuhusu uwezekano wa kutokea shambulio katika eneo hilo.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.