Zaidi ya walimu 20,000 waliofeli mtihani wa wanafunzi wao kufutwa Kazi
Mamlaka katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kaduna zinasema kuwa zaidi ya walimu 20,000 wa shule za msingi watafutwa baada ya wao kufeli mtihani unaotahili kufanywa na wanafunzi wao.
Hii inafuatia madai kuwa nyingi ya shule za msingi na sekondari nchini Nigeria huzalisha wanafunzi wasiohitimu vyema.
Gavana wa jimbo la Kaduna el-Rufai alisema kuwa walimu waliohitimu wataajiriwa kuchukua mahala pa wale watakaofutwa.
Haijulikani hatua hii itachukuliwa lini.
Afisa mmoja wa cheo cha juu katika jimbo la Kaduna aliambia BBC kuwa mitihani zaidi itatolewa siku zinazokuja kwa walimu wa sekondani.
Wadadisi wanasema kuwa idadi hiyo ni ishara ya viwango duni vya elimu nchini Nigeria ambapo inadaiwa kuwa walimu huajiriwa kwa misingi ya kisiasa.
BBC
No comments: