Header Ads

ad

Elias Maguli anukia Jangwani…..

Baada ya kuzagaa tetesi kuwa mshambuliaji anayecheza soka la kulipwa nchini Oman, Elius Maguri yuko mbioni kujiunga na Yanga hatimaye Katibu mkuu wa mabingwa hao Boniface Mkwasa amefunguka na kusema muda ukifika kila kitu kitakuwa hadharani.
Mkwasa hakukanusha wala kukubali kuwa wako kwenye mbio za kumuwania mchezaji huyo wa zamani wa Simba zaidi ya kusema kama watamsajili au la itafahamika na kila mtu atajua.
Maguri ambaye alifunga bao la kusawazisha la timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ dhidi ya Benin ugenini wiki iliyopita amejumuishwa katika kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Kilimanjaro heroes itakayo shiriki michuano ya CECAFA Chalenji mwezi ujao nchini Kenya.
“Maguri ni Mtanzania na ana sifa ya kuchezea Yanga, kama atasajiliwa au hatasajiliwa ni suala la kusubiri na kuona,” alisema Mkwasa.
Yanga imekosa huduma ya washambuliaji wake Amiss Tambwe na Donald Ngoma ambao ni majeruhi kwa muda mrefu hivyo wanamuona Maguri kama mbadala wa nyota hao raia wakigeni.
Tayari dirisha dogo la usajili limefunguliwa Novemba 15 litakalo malizika Disemba 15 mwaka huu huku kila timu ikiwa nafasi ya kuongeza wachezaji katika mapungufu yaliyojitokeza katika mechi zilizopita.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.