Header Ads

ad

ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA NA KULAWITI WATOTO


Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, linamshikilia kijana mmoja mwenye umri wa miaka 30 kwa tuhuma za kuwabaka watoto wanne.

Tukio hilo limeripotiwa kutokea siku ya Ijumaa, Disemba 8 mwaka huu ambapo mtuhumiwa anadaiwa kuwabaka na kuwalawiti watoto hao ambao wana umri chini ya miaka 18.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja, Makharani Khamis alieleza kuwa awali mtuhumiwa alidaiwa kuwabaka na kulawiti watoto saba lakini uchunguzi wa daktari ulibaini kuwa ni wanne peke yake ndio walioathiriwa huku watatu wakiwa salama.

Aliendelea kwa kusema kuwa mtuhumiwa amekuwa akifanya vitendo hivyo kwa watoto hao nyakati tofauti tofauti na kuongeza kuwa mtuhumiwa kwa sasa yukorumande huku uchunguzi ukiendelea na atafikishwa katika vyombo vya sheria pale utakapokamilika.

Alieleza kuwa watoto hao walitambuliwa kufanyiwa vitendo hivyo baada ya mzazi mmoja kubaini kuwa mwanae ana harufu mbaya na alipomhoji ndipo alipomtaja mtuhumiwa na kueleza kuwa mtuhumiwa amekuwa akiwafanyia hivyo yeye na watoto wenzake huku akiwapa fedha kiasi cha shilingi 5,000 ili wasiseme.

Kamanda MAkharani ameitaka jamii kutokuwaacha watoto mbali, bali wawe karibu nao na kufuatilia mienendo yao ili kubaini kama kuna vitendo vibaya wanavyofanyiwa.
Aidha aliwataka wazazi na walezi kuwa na tabia ya kuwachunguza watoto wao ikiwemo kuwaogesha ili kubaini kama kuna dosari yoyote katika miili yao na watakapobaini wafanye uchunguzi na watoe taarifa kwa vyombo husika ili sheria ichukue mkondo wake badala ya kubaki wanalalamika tu mtaani.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.