Header Ads

ad

RAIS MAGUFULI AVIONYA VYOMBO VYA HABARI NA MITANDAO YA KIJAMII


Rais wa Jamhuri ya muungano wa tanzania, john Pombe Magufuli, amevionya vyombo vya habari na wamiliki wa mitandao ya kijamii kuacha kutoa takwimu za kupotosha iwe ni kwa malengo ya kisiasa ama kwa lengo lingine lolote.

Nawaonya vyombo vya habari na wataalamu wa mitandao, tusitafute takwimu za kupika,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo katika hotuba aliyoitoa katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi jengo la ofisi ya Taifa ya Takwimu mjini Dodoma na kuzitaka mamlaka husika kuwachukulia hatua wale wote wanaotoa takwimu za uongo tofauti na zinazotolewa na ofisi ya takwimu.

Naagiza mamlaka kuwachukulia hatua wote wanaotoa takwimu za uongo tofauti na zinazotolewa na ofisi ya takwimu,” amesema Rais Magufuli.
Rais amesisitiza kuwa sheria ya takwimu iko wazi na kueleza kuwa adhabu zake zinaeleweka ambayo ni kifungo kisichopungua miezi 6 hadi miaka mitatu, faini ya shilingi milioni moja hadi milioni 10 au vyote viwili.

“Sheria ya takwimu kifungu cha 37 kifungu kidogo cha 3 mpaka 5 kinaeleza kuwa mtu au taasisi yoyote ikitoa takwimu za uongo, adhabu yake ni kifungo kisichopungua miezi 6 hadi miaka mitatu jela, au faini ya kuanzia shilingi milioni 1 hadi milioni kumi, au vyote kwa pamoja,” amesisitiza Rais Magufuli.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.