Header Ads

ad

TAARIFA KUHUSU MAPOKEZI YA ZANZIBAR HEROES


Timu ya Taifa ya Mpira wa Miguu ya Zanzibar maarufu Zanzibar Heroes itarejea Visiwani Zanzibar kesho Jumatatu tarehe 18/12/2017 saa 3:00 asubuhi ikitokea nchini Kenya ilikokuwa ikishiriki mashindano ya Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA Senior Challenge Cup’ 2017)

Zanzibar Heroes itapokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume na Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi.
Zanzibar Heroes imeshika nafasi ya pili katika michuano hiyo baada ya Kenya kupata ushindi wa penalti 3-2 kufuatia sare ya 2-2 ndani ya dakika 120 Uwanja wa Kenyatta mjini Machakos.

Mlinda mlango wa Kenya, Matasi alipangua penati za Adeyoum Ahmed, Issa Haidari ‘Dau’ na Mohammed Issa ‘Banka’ huku penati mbili tu za viungo Feisal Salum Abdallah na Mudathir Yahya Abbas zikitinga wavuni.
Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, bingwa mtetezi Uganda iliichapa Burundi mabao 2-1 katika Uwanja wa Kenyatta, Machakos.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.