Header Ads

ad

WASIFU WA AKWILINA AKWILIN ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI

Akwilina Akwilini alizaliwa tarehe 1 April, 1996 katika Kijiji cha Olele-Marangu, wilayani Rombo, mkoani Kilimanjaro, akiwa ni mtoto wa sita kati ya watoto nane wa familia ya mzee Akwilini Shirima.

Akwilina alipata sakramenti mbalimbali katika kanisa Katoliki la Kitongoria. Sakramenti hizo ni pamoja na Ubatizo, komnyo ya kwanza na sakramenti ya kipaimara.
Marehemu Akwilina alisoma darasa la kwanza mpaka la saba mwaka 2004 – 2010, katika shule ya msingi Kitongoria.

Alijiunga na kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2011 – 2014, katika Shule ya Sekondari ya Higland iliyopo mkoani Iringa.
Akwilina aliendelea na kidato cha tano na cha sita katika shule ya Embarai Arusha na baadae Lugalo High School iliyopo mkoani Iringa.

Umahiri na uadilifu katika elimu yake ulimfanya Akwilina kujiunga na Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji, Oktoba 30, 2017 akiisaka shahada ya Ugavi na Usafirishaji NIT.
Akwilina alifariki kwa kupigwa risasi akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Wilaya ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kukutwa na umauti, Akwilina aliwaaga wanafunzi wenzake kuwa anakwenda Bagamoyo kufanya maandalizi ya sehemu ya kufanyia field siku ya Ijumaa tarehe 16 februari, 2018.

Katika tukio hilo ambalo lilipelekea kuchukua uhai wa mwanafunzi Akwilina, polisi walikuwa wakiwatawnya waandamanaji wanaosadikiwa kuwa ni wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), waliokuwa wakifanya maandamano siku moja kabla ya uchaguzi mdogo mbunge katika Jimbo la Kinondoni.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.