Header Ads

ad

Rais Magufuli amlilia Abbas Kandoro

Leo April 27, 2018 Rais Magufuli ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekuwa RC wa zamani, Abbas Kandoro kilichotokea jana April 27, jioni katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.

“Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Mkoa Mstaafu Abbas Kandoro, nawapa pole wana familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu, pamoja na wananchi wa mikoa ya Tabora, Arusha, Dar es Salaam, Mwanza na Mbeya ambako aliwahi kuwa Mkuu wa Mkoa.” -Rais Magufuli

“Tumempoteza mtu muhimu ambaye mchango wake katika utumishi kwa umma katika nyadhifa mbalimbali zikiwemo Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi wa halmashauri hautasahaulika.” -Rais Magufuli

“Abbas Kandoro alikuwa kiongozi shupavu, aliyejiamini na kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria na taratibu, aliwapenda watu aliowaongoza na alidhirisha uzalendo wa kweli.” -Rais Magufuli

“Nimesikitishwa sana na kifo chake, nawaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira, uvumilivu na ustahilivu katika kipindi hiki cha majonzi na pia namuombea Marehemu Abbas Kandoro apumzike mahali pema peponi, Amina” -Rais Magufuli

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.