Manula Kuwakosa Kagera Sugar
KIPA namba moja wa timu ya Simba, Aishi Manula ataukosa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom dhidi ya Kagera Sugar ambao umepangwa kutumika kuwakabidhi kombe Wekundu hao wa Msimbazi.
Aishi atakuwa jukwaani akiishuhudia timu yake ikipambana kuipamba siku hiyo muhimu kwao kwavile anatumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.
Kipa huyo aliyecheza kwa kiwango cha juu msimu huu alionyeshwa kadi ya njano (ambayo ni ya tatu msimu huu) katika mchezo wa jana walioshinda bao 1-0 dhidi ya Singida United kwa kosa la kupoteza muda.
Simba inauchukulia kwa uzito wa juu mchezo huo kwani wamedhamiria kumaliza ligi bila kupoteza hata mchezo mmoja huku pia wakihakikisha Kagera hawaimwagii mchanga pilau yao.
No comments: