SIMBA, YANGA, AZAM ZAFUNIKA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA VPL, ORODHA KAMILI HII HAPA
Timu tatu za Simba, Yanga na Azam zimeongoza kwa kutoa wachezaji wengi zaidi kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu unaomalizika wa 2017/18.
Kwa mujibu wa orodha ya awali ya wachezaji hao iliyowekwa hadharani leo na kamati ya tuzo, timu hizo tatu zimetoa jumla ya wachezaji 17, ambapo mabingwa wapya wa ligi hiyo Simba wametoa wachezaji saba, huku Yanga na Azam zikitoa wachezaji watano kila mmoja.
Mbali na timu hizo tatu, timu nyingine zilizotoa wachezaji kwenye orodha hiyo ni Singida United wachezaji watatu, Mtibwa Sugar wachezaji wawili huku timu za Mbeya City, Majimaji, Njombe Mji, Mbao FC, Ruvu Shooting, Lipuli FC, Mwadui FC na Tanzania Prisons zikitoa mchezaji mmoja mmoja.
Kati ya timu 16 za VPL, ni timu tatu pekee ambazo hazijatoa mchezaji hata mmoja. Timu hizo ni Stand United, Ndanda SC na Kagera Sugar. Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, wachezaji hao watachujwa na kubaki 10, kisha watabaki watatu ambao ndiyo wataingia fainali ya kuwania tuzo siku ya mwisho katika sherehe zitakazofanyika Juni 23, kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Orodha kamili ya wachezaji hao ni kama ifuatavyo:- Habibu Kyombo (Mbao), Khamis Mcha (RuvuShooting), Yahya Zayd (Azam), Razack Abalora (Azam), Bruce Kangwa (Azam), Aggrey Morris (Azam), HimidMao (Azam), Awesu Awesu (Mwadui), Adam Salamba (Lipuli), Mohammed Rashid (Prisons), Shafiq Batambuze (Singida United, Mudathir Yahya (Singida United), Marcel Kaheza (Majimaji), Ditram Nchimbi (Njombe Mji), Eliud Ambokile (Mbeya City), Wengine ni Shaaban Nditi (Mtibwa), Tafadzwa Kutinyu (Singida United), Ibrahim Ajibu (Yanga), Gadiel Michael (Yanga), Papy Tshishimbi (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Obrey Chirwa (Yanga), Aishi Manula (Simba), Emmanuel Okwi (Simba), John Bocco (Simba), Jonas Mkude (Simba), Erasto Nyoni (Simba), Shiza Kichuya (Simba), Asante Kwasi (Simba), Hassan Dilunga (Mtibwa).
No comments: