Header Ads

ad

Wabunge wawafundisha Maaskofu mgomo

Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni imeliomba Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) kutoijibu barua waliyopewa na Serikali ikiwa ni pamoja na kuitaka Serikali kuwaomba radhi waumini wa madhehebu hayo mawili.

Upinzani umetoa kauli hiyo ya pamoja leo katika mkutano wailioufanya na waandishi wa habari katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.
Akizungumza kwa niaba ya Wabunge wenzake, Mbunge wa Vunjo James Mbatia amesema Waziri Mkuu ndiyo msimamizi na mdhibiti wa shughuli za Serikali bungeni na swali lililoulizwa leo lilitaka kupata majibu kuhusu hatima ya KKKT na Katoliki.
Wabunge hao wa upinzani wamesema kuanzia sasa watahakikisha wanatumia mbinu mbalimbali ndani ya Bunge kuitaka Serikali kutoa majibu ya kina kuhusu barua hizo hususani kuifuta barua yake.

“Wasiwajibu Serikali halafu waone Serikali itachukua hatua gani kwani nchi hii si mali ya Serikali. Waumini wako katika hamaki, viongozi hawa wa dini ni Watanzania na wana haki ya kutoa maoni, Serikali inapaswa kuwaomba radhi waumini.” Mbatia.

Swali la Mbatia kwenda kwa Waziri Mkuu kohoji kuhusu Serikali kutoa siku 10 kwa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kufuta waraka wake Pasaka uliotolewa Machi 24, 2018, lilizuiliwa majibu na Naibu Spika Tulia Ackson kwa madai kuwa wali hilo haliwezi kujibiwa na kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.

Kwa upande wake Kaimu Kiongozi wa Upinzani Bunngeni, Abdallah Mtolea amesema “Tumeamua kuyasema haya, yanayofanyika kwa kuwa yanakwenda kuivuruga nchi hii, taasisi hizi zinaongozwa na viongozi wa kiroho wanaoaminika kuliko sisi wanasiasa, Serikali iache kuingilia hizi taasisi, iache kuwaingilia pale wanaposema wanachanganya masuala ya siasa.

Barua inayosambaa katika mitandao ya kijamii imetaka Kanisa la KKK kufuta waraka walioutoa kipindi cha pasaka ndani ya siku kumi kuanzia Mei 30, 2018, pamoja na waraka wa  TEC uliotolewa wakati wa Kwaresma.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.