Header Ads

ad

Simba yaingia vitani, kuipeperusha bendera

Mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC imeingia vitani baada ya kufanikiwa kutinga fainali za michuano ya Sports Pesa super Cup ikiungana na mabingwa wa tetezi wa kombe hilo Gor Mahia ya Kenya ambapo bingwa atakipiga na Everton katika Dimba la Goodson Park.

Simba ilikuwa ya kwanza kufika fainali kwa ushindi wa mabao 5-4 yaliyopatikana kwa changamoto ya mikwaju ya penati baada ya dakika 90 kwenda suluhu tasa ya 0-0 dhidi ya Kakamega HomeBoyz FC.

Singida United imeshindwa kufuzu kucheza fainali ya Super Cup nchini Kenya kwa kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Gor Mahia FC kwa mabao 2-0 ambayo itakutana na Kakamega HomeBoyz FC kusaka nafasi ya tatu.

Aidha mabingwa hao wa Tanzania watalazimika kuondoka Jumapili baada ya fainali hiyo huku wakiwahi tuzo za Mo Simba Awards zinazotarajiwa kutolewa Juni 11 mwaka huu.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.