Header Ads

ad

Jaji Mkuu amshtumu IGP


Jaji Mkuu wa Kenya, David Maraga, amemshutumu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo, IGP, Joseph Boinet, kwa kukataa wito wa kuimarisha usalama wa Majaji na Mahakama hivyo kuhatarisha usalama wao.

Katika taarifa baada ya mkutano na wanachama wa Tume ya Huduma za Mahakama, JSC, Bw. Maraga, amesema, licha ya hali hiyo, Idara ya Mahakama na Majaji wataendelea kutoa huduma zake.
Amesema, wako tayari kukabiliana na lolote lile kutetea Katiba na Sheria ya Kenya na kusisitiza kuwa, Idara ya Mahakama ni kitengo huru cha serikali sawa na uongozi wa taifa na Bunge.
Amesema, iwapo viongozi wamechoka kuwa na Idara ya Mahakama iliyo thabiti na huru, waitishe kura ya maamuzi na kuifutilia mbali.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.