Header Ads

ad

Wanaouza dawa za nguvu za kiume bila kufuata sheria kukamatwa

Serikali imepiga marufuku waganga wa tiba za asili nchini na wadau mbalimbali ambao wanauza dawa zinazodaiwa kuongeza nguvu za kiume kinyume na sheria.

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema hayo Jumatano hii Bungeni Dodoma wakati akijibu swali ya mbunge aliyetaka kujua serikali inachukua hatua gani kwa waganga wa jadi ambao wanaotembeza dawa barabari wakidai zinaongeza nguvu za kiume.

“Wale ambao wanauza dawa za nguvu za kiume bila kufuata utaratibu tutawakamata na kuwachulia hatua, hiyo ndio kauli ya serikali wanaofanya hivyo wanafanya kinyume na sheria na kutumia bunge lako tukufu Mh Naibu Spika niwatake waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuwachukulia hatua watu wote wanaouza dawa za kuongeza nguvu za kiume ambazo hazijasajiliwa na mamlaka ya tiba asili au tiba mbadala,” alisema Ummy Mwalimu.
Waziri huyo amewataka wadau hao kufuata taratibu ambazo zimewekwa na serikali katika kutoa tiba asili.
Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.