Header Ads

ad

Kauli za Nape Nnauye


Mbunge wa jimbo la Mtama, Mh Nape Nnauye toka umeanza mwezi Oktoba, 2017 ametoa kauli zake tatu ambapo katika kauli ya kwanza alikuwa amelenga kuwapa ujasiri vijana na Watanzania kiujumla kuchukua hatua katika mambo fulani fulani.

Nape Nnauye alitumia mtandao wake wa twitter kuyasema hayo na kuwambia kuwa unapoona umekosa matumaini juu ya jambo fulani hupaswi kusita kufanya maamuzi huku ukimuamini Mungu kwani yeye hutoa njia.

"Mwenyezi Mungu hufanya njia pasipokuwa na njia! Amini na chukua hatua" alisema Nape Nnauye

Aidha Mbunge huyo alizidi kuwasisitiza Watanzania na kuwataka kuwa na busara katika mambo yao hata mambo yanapokwenda ndivyo sivyo aliwataka kutumia busara zaidi "Taulo likianguka, hatua ya kwanza chutama, ndio busara aaaakh" alisema Nape Nnauye
Mbali na hili Nape Nnauye alimalizia kwa kauli hii "Usipande miba kwenye njia yangu maana unaweza kesho kuja kwangu ukiwa peku! Weka akiba"

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.