CUF yaionya CCM
Chama cha wananchi CUF, kimetoa msimamo wake kuhusu uchaguzi mdogo wa madiwani kwamba hakitakurupuka kutoa wagombea bali watashirikina vema na UKAWA ili kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa kwenye vyama vya upinzani na siyo kuipa ushindi CCM.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari, Uenezi na Mahusiano Na Umma-CUF Taifa upande wa Maalim Seif, Naibu Mkurugenzi Maharagande Mbarala inasema kwamba anawataka viongozi na wanachama wote makini walipuuze genge la Lipumba na kwamba CUF haitasita kuongeza nguvu zake kwa kushirikiana na upinzani wengine katika kata watakazo zimamisha wagombea wao ili kufanikisha ushindi kwa vyama vya upinzani katika maeneo yatakayoainishwa.
Taarifa inasema kwamba CUF haitafanya maamuzi ya kukurupuka, itazingatia vigezo vya matokeo ya Chaguzi zilizopita 2015/2017, kwamba Kata ilikuwa inaongozwa na Chama gani kabla ya uchaguzi kama Kata ilikuwa inaongozwa na NCCR au CHADEMA hakuna sababu ya CUF kusimamisha Mgombea eneo hilo na kinyume chake kwenye ngome za CUF hakuna sababu vyama vingine kusimamisha wagombea wao.
Ameongeza kwamba Kurugenzi ya Mipango na Uchaguzi CUF Taifa inaendelea kufanya mawasiliano na viongozi wa chama wa maeneo husika na kupitia ‘Database’ yake kwa kufanya uchambuzi yakinifu ili itoe taarifa sahihi kwa maslahi mapana ya CUF, upinzani na watanzania Wwapenda mabadiliko kwa ujumla.
Mbali na hayo Mbarala ameonya na kusema kwamba taarifa zilizotolewa na vibaraka wa CCM kwamba CUF itawasimamisha wagombea katika kata zote 43 zinazorudia uchaguzi ni za uongo na kupuuzwa kwani CUF haikuundwa kuwa Chama cha kuisadia CCM iendelee kutawala Tanzania.
No comments: