Baraza la Mawaziri labadilishwa... Maghembe Atupwa Nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amefanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri na kuongeza wizara mbili, hivyo kufikia wizara 21 kutoka 19 ambazo zilikuwepo.
Tukio hilo limetokea leo ambapo Rais Magufuli pia amezigawa Wizara ya Kilimo, Mifugo, Uvuvi na kuwa wizara ya Kilimo pekee na Wizara ya Mifugo na Uvuvi peke yake, pamoja na Wizara ya Nishati na Madini kuwa wizara mbili tofauti.
Sambaba na hilo pia Rais Magufuli amemteua Mh. George Haruna Mkuchika kuwa Waziri Ofisi ya Rais Utawala Bora, ambaye kabla alikuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Mawaziri hao wanatarajiwa kuapishwa siku ya jumatatu Oktoba 9, 2017, Ikulu jijini Dar es salaam.
No comments: