TUNDU LISSU AWATAJA WALIOHUSIKA KATIKA KUMSHAMBULIA
Tundu Lissu ambaye ni mara yake ya kwanza kuongea katika mahojiano na chombo cha Habari amelieleza jarida la ‘Financial Times Kenya’ kuwa serikali inalenga kuvinyamazisha vyama vya upinzani, vyombo vya habari, taasisi za kijamii, vyama vya wafanyakazi pamoja na makanisa.
Tundu lissu alieleza kuwa sekunde chache baada ya watu waliomshambulia kuruka kutoka kwenye gari ambayo aliiripoti kuwa inamfuatilia kwa zaidi ya wiki tatu, dereva wake alimlaza kwenye sakafu ya gari ili kumuokoa dhidi ya shambulizi hilo.
“Nimeambiwa kwa sababu sikuweza kuhesabu, kuwa risasi 38 zililipata gari langu na kati ya hizo, risasi kama 16 hivi ziliniingia mwilini” alisema Tundu Lissu ambaye ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni.
Msemaji Mkuu wa Serikali, Hassan Abbas amekanusha vikali madai ya Tundu Lissu.
Aidha matukio ya mauaji ni machache katika Afrika Mashariki, na Rais Magufuli alisikitishwa na tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu na kusema kuwa ni tukio la kinyama huku akivitaka vyombo husika kuchukua hatua.
Hata hivyo Jeshi la Polisi bado halijazungumza chochote kuhusiana na uchunguzi juu ya tukio hilo japokuwa eneo la nyumba ya Tundu Lissu ambapo ndipo lilipotokea shambulio hilo linalindwa na kamera za ulinzi za ‘CCTV’.
No comments: