LULU AKUTWA NA KESI YA KUJIBU KATIKA SHTAKA LA KUMUUA KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo Oktoba 23 imemkuta na kesi ya kujibu msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu, Lulu baada ya mashahidi wanne wa upande wa Jamhuri kumaliza kuwasilisha ushahidi wao mbele ya mahakama.
Lulu amekutwa na kesi ya kujibu katika shtaka la kuua bila kukusudia linalomkabili.
Katika kesi ya msingi, Lulu anatuhumiwa kumuua bila kukusudia aliyekuwa msanii mwenzake wa filamu nchini Tanzania, Steven Kanumba Aprili mwaka 2012.
No comments: