MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA BIASHARA YENYE MAFANIKIO
Kuanzisha biashaara au kampuni ni jambo jema kwa kila mjasiriamali. Lakini jambo la msingi kufahamu ni njia gani bora ya kuianzisha biashara.
Waanzilishi wa kampuni pasipo kutambua hujikuta wanafanya maamuzi ambayo ndiyo yatakayopelekea kupata mafanikio ama kutokufanikiwa kwa biashara.
Ki ukweli, unapoanzisha biashara mpya, lazima ukumbane na ugumu pamoja na changamoto mablimbali. Lakini usijali, endelea kupambana na kuongeza juhudi ili kuyafikia malengo uliyojiwekea.
Kama umeamua kuanzisha biashara yako (ama unamfahamu mtu ambaye anataka kuanzisha biashara) inakupasa kusoma mambo yaliyoorodheshwa hapo chini. Unaweza ukaona ugumu kuyafikia mambo yote yaliyotajwa, lakini jitahidi kufikia mengi kadiri ya uwezo wako ili kuifanya biashara yako kuwa bora.
Biashara bora hailengi kuuza katika soko la ndani tu (lical Market), lakini pia katika masoko ya kimataifa.
Aidha, bidhaa haiwezi kubadilishwa kwa urahisi au kunakiliwa.
Biashara bora haihitaji kuajiri wafanyakazi wengi au wewe kuwekeza sana katika nguvu kazi. Unapaswa kuwa na ofisi ambayo itakuwa na watendaji tu. Uzalishaji, masoko na usambazaji utafanywa na kampuni nyingine.
Biashara bora siyo lazima iwe na uwekezaji mkubwa. huhitaji ofisi kubwa na ya gharama, huhitaji nishati kubwa, huhitaji wafanyakazi wengi wala mtaji mkubwa. Kikubwa hapa ni ubunifu tu.
Biashara bora haihitaji uwekezaji mkubwa katika vitendea kazi. Hivyo mtaji mkubwa siyo chanzo cha biashara bora. Japo unachangia kwa kiasi fulani.
Lengo la biashara katika kampuni yako ni kutengeneza faida. Hivyo hatutegemei kuwa biashara yako itaendeshwa kwa mikopo mingi.
Taratibu za kiserikali haziingiliani na biashara yako kwa kiwango kikubwa. Acha woga.
Biashara bora ni rahisi kuhamia maeneo mengine.
Biashara bora hukupa hamasa kiakili na utaifurahia.
Biashara bora hukupa muda wa kutosha kufikiri namna ya kuitanua na kuiongeza biashara yako tofauti na unapofanya kazi ya mtu mwingine, unakuwa unafanya kazi kubwa ili kufikia malengo yake.
No comments: