MARAIS 10 WA AFRIKA WANAOLIPWA MISHAHARA MIKUBWA ZAIDI
Kitendo cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutaja kiwango cha mshahara anaolipwa kwa mwezi kimewasisimua wengi
Rais Magufuli alitaja kiwango anacholipwa kama mshahara wake kuwa ni shilingi za kitanzania milioni 9 katika hotuba yake wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 33 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa (ALAT) katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam, tarehe 03 Oktoba, 2017.
Kiwango hicho cha mshahara wa rais wa Tanzania kimekuwa ndicho kiwango kidogo zaidi kikilinganishwa na viwango wanavyolipwa maraisi wengine wa Afrika Mashariki.
Rais anayeongoza kwa mshahara mkubwa Afrika Mashariki ni Yoweri Museveni anayelipwa Tsh 32.6m kwa mwezi akifuatiwa na Kenyatta Tsh 30.4m kisha Kagame, anayelipwa takribani Tsh 15.2m.
Kwa Afrika, kiwango cha mshahara anacholipwa Rais Magufuli ni pungufu mara 10 ya mshahara anaolipwa Rais wa Cameroon.
Rais wa Cameroon, Paul Biyandiye kiongozi anayelipwa mshahara mkubwa zaidi Afrika, ambapo yeye analipwa Tsh. 114.2 milioni kwa mwezi na amekaa madarakani kwa muda wa miongo mitatu na nusu mpaka sasa.
Rais wa Sierra Leone, Ernest Bai Koroma ndiye anayelipwa mshahara mdogo kuliko wengine Afrika, ambapo analipwa Tsh. 2.2 milioni kwa mwezi.
No comments: