MBUNGE AKOSEA NA KUTUMA UJUMBE WA NGONO KWENYE KUNDI LA WHATSAPP
KENYA: Mbunge wa Jimbo la Mukurwe-ini nchini Kenya amewashtua wapiga kura wake baada ya kutuma ujumbe wa masuala ya ngono katika kundi la WhatsApp la jimbo lake.
Mbunge Anthony Kiai alituma ujumbe wa maneno katika kundi hilo ambao ulikuwa unaelezea namna ya kumridhisha mwanamke unapofanya naye mapenzi.
Ujumbe huo ambao ulitumwa katika kundi lenye jina la “ Mukurwe-ini Newsroom Group” haukuishia hapo bali ulielezea pia mambo ambayo mwanaume anatakiwa kufanya baada ya kujamiiana na mwanamke.
Baada ya kubaini kuwa amekosea kutuma ujumbe huo, mbunge huyo aliwataka wajumbe wa kundi hilo kuupuuza ujumbe huo, lakini wao walishinikiza awaombe msamaha kwa kutoa lugha isiyo stahiki.
Picha (screenshots) za ujumbe huo zimesambaa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii na kuzua maswali mengi miongoni wa raia wa Kenya.
Mbali na wengi waliomkosoa mbunge huyo, wengine walimtetea na kusema kwamba hawaoni tatizo la ujumbe huo kwa sababu kujamiiana sio dhambi.
Tulimchagua binadamu mwenye hisia na wala si malaika, mimi sioni tatizo la ujumbe huu kwani wote tunajamiiana na alichosema ni cha kweli, labda kama tunataka kujidanganya kwamba maisha yetu ni kamili sana, alisema mjumbe mmoja.
Aidha, msaidizi wa mbunge huyo aliomba radhi kwa niaba ya kiongozi huyo.
Mbunge huyo hakuweza kupatikana kuzungumzia sakata hilo lililoibua mvutano mkali.
No comments: