Header Ads

ad

PICHA YA KWANZA YA TUNDU LISSU KUTOLEWA AKIWA HOSPITALINI NAIROBI


Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa mara ya kwanza kimetoa picha ya Mbunge Tundu Lissu anayepatiwa matibabu jijini Nairobi nchini Kenya tangu aliposhambuliwa kwa risasi akiwa Dodoma Septemba 7 mwaka huu.

Picha hizi zimetolewa baada ya jana Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kusema kuwa saa chache zijazo watanzania wataweza kumuona na kumsikia Tundu Lissu akizungumza.

Mbowe aliyesema hayo jana katika Ofisi za Makao Makuu ya CHADEMA wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo afya ya mbunge huyo aliyeshambuliwa kwa risasi baada ya kutoka kwenye kikao cha Bunge eneo la Area D mjini Dodoma.

Katika taarifa yake, Mbowe alisema kuwa Afya ya Lissu sasa imeimarika kwani mashine zote zilizokuwa zikimsaidia zimeondolewa baada ya mwili wake kuimarika na kwamba sasa anaweza kula mwenyewe, na mwishoni mwa juma alitolewa nje akiwa kwenye kiti cha wagonjwa na kuliona jua kwa mara ya kwanza.

Mbowe aliwaeleza watanzania kuwa baada ya awamu ya kwanza na ya pili ya matibabu ya Lissu kukamilika, itafuata awamu ya tatu ambayo matibabu yake yatakuwa nje ya Nairobi, lakini hakusema ni wapi kutokana na sababu za kiusalama.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.