Shahidi afichua mapya ya Kanumba
Kesi inayomkabili Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu', imeendelea leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambapo ushahidi wa upande wa utetezi uliokuwa ukisubiriwa umewasilishwa na kusomwa na Polisi Detective Sergeant Nengea aliyerekodi
ushahidi huo kutoka kwa aliyekuwa Daktari wa Marehemu Steven Kanumba.
Katika ushahidi uliosomwa na Sergeant Nengea (ambaye mahakama imemtambua kama shahidi) ambao aliurekodi kutoka kwa Josephine Mushumbusi umedai kwamba "Marehemu alikua na matatizo ya damu, upungufu wa hewa kwenye ubongo, alikuwa anasikia maumivu katika ubongo na akili kuchoka".
Aidha ushahidi huo umekamilisha kesi hiyo siku ya leo lakini Wakili Kibatala ameiomba mahakama kumruhusu kumpatia nafasi ya kutoa hoja za ziada ambazo zitasaidia katika kufanya maamuzi juu ya kesi hiyo.
Hata hivyo Jaji Sam Rumanyika amesema kesho wazee wa baraza watakaa na kujadili kama Lulu ana hatia katika kesi hiyo inayomkabili au hana, na kusubiria kupanga siku ya hukumu.
No comments: