MANARA AMTOSA AJIBU
Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amefunguka na kuweka wazi kuwa ni kweli Mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajibu Migomba kwa sasa ni kiburudisho tosha nchini lakini amemtosa kuwa mshambuliaji huyo huwezi kumfananisha na Okwi.
Haji Manara amesema hayo kupitia mtandao wake wa kijamii na kusema ni kweli aliwahi kutamka hilo lakini ukweli unabakia pale pale kuwa kwa sasa Ajib bado huwezi kumfananisha na Okwi kwani wanatofauti kubwa ndiyo maana hata idadi ya magoli yao imekuwa kubwa kati yao.
"Ni kweli niliandika Ajibu ni kiburudisho zaid nchini kwa sasa, ila ninaendelea kukemea kashushwa na Mungu ndio imani yangu itakavyo. Kisha sisi tunataka ubingwa, viburudisho peleka kwenye minuso, ndio maana tuna Okwi kama mbadala wa viburudisho, goli nane kwa tano wapi na wapi" aliandika Manara
Mshambuliaji wa Simba Emmanuel Okwi kwa sasa ndiye anayeongoza kwenye Ligi Kuu Bara kwa kuwa na idadi kubwa ya magoli ambayo ni 8 akifuatiwa na mshambuliaji kutoka Yanga Ajib ambaye ana magoli 5 kwa mechi 7 walizocheza.
Simba na Yanga zinatarajiwa kukutana Jumamosi hii Oktoba 28, 2017 katika mzunguko wa nane wa Ligi Kuu Tanzania Bara
No comments: