UFAFANUZI WATOLEWA KUHUSU GARI ALILOLITUMIA MAKONDA AKIWA ZANZIBAR
UNGUJA: Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mahmoud ameeleza kusikitishwa kwake na taarifa zisizo za kweli zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kuhusu gari alilolitumia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alipokuwa ziarani mkoa humo.
Mahmoud ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram, baada ya kuwepo kwa taarifa mbalimbali kuhusu gari aina ya Range Rover ambayo ilikuwa na namba za usajili zinazoonyesha kuwa ni la RC Dar es Salaam.
“Unaweza ukasikitishwa sana pale unapoona chombo kinacho aminiwa kwenye maswala ya habari kuwa ni chanzo cha upotoshaji!. No research no right to speak !.”
RC Mahmoud aliendelea kueleza kuwa, “Hii sio gari ya serekali au ya ndugu yangu Paul Makonda! Kilichokuwepo ni nini? In fact hakuna asojua kuwa ndugu yetu Paul yuko Zanzibar na Mimi nikiwa kama mwenyeji wake ndani ya mkoa wangu!.”
RC Mahmoud alisema kwamba, kinachosumbua watu kuhusu gari hilo, ni watu kutokufahamu taratibu zinazo wahusu viongozi hao.
“Hii ni gari ya mtu binafsi imetumika kwa mdaa wakati ule wote wa Mkuu wa mkoa wa dar es Salaam kuwa zanzibar katika kilele cha mbio za mwenge na maadhimisho ya kifo cha Baba wa taifa pamoja na ziara yake katika mkoa wa mjini magharibi!.”
Kwa upande wake RC Makonda alisema kwamba, sio kwamba watu wanaozusha habari hizo hawajui ukweli, bali wanakerwa na upendo ambao ameonyeshwa na kiongozi huyo akiwa ziara Mjini Magharibi.
“Mhe Rc na Kaka yangu mpendwa . Hawa Watu wanajua wanachokifanya na wanaelewa kabisa kwamba nilikuwa Zanzibar. Wanachoumia ni upendo na ukarimu wako na watu wako wa unguja kwangu. Tuchape kazi maneno niyao.”
No comments: