Header Ads

ad

Makamu wa Rais awachana wanaume


Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu amewataka wanaume wa Tanzania kuacha kuwa na mahusiano ya kimapenzi na watoto wadogo, kwa kuona wakubwa wenzao hawana ladha ile wanayoitaka

Mama Samia ametoa kauli hiyo wakati wa maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani,na kusema kwamba kitendo cha wanaume hao kuwafuata watoto wadogo licha ya kujua wameambukizwa ili tu kupata ladha yao, ni dhambi kubwa ambayo hata Mungu hawezi samehe.

" Wanaume na nyinyi muwe na maadili, wanaume wakubwa mnahisi labda wakubwa wenzenu wamechuja hawana ladha ile ambayo mngependa kuipata, kwa hiyo mnahamia kwa wototo wadogo, huu si mwendo mzri, hawa ni watoto wetu, hili ni taifa la kesho, na wengine wanaijua kabisa kwamba wameshaambukizwa, na wakubwa wenzao wanajua wameambukizwa, wanashifti kwa watoto ambao hawawajui kwa kutumia vicent kidogo, huu ni uuaji wa makusudi na Mungu hatawasamehe katika hili waachieni watoto wetu wakue watunze taifa letu ", amesema Mama Samia.

Hapo jana dunia imeadhimisha siku ya UKIMWI, ambapo sherehe hizo kitaifa zimefanyika jijini Dar es salaam katika viwanja vya mnazi mmoja, na Makamu wa Rais kuhudhuria kama mgeni rasmi.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.