Header Ads

ad

Niyonzima amerudi Simba

Kiungo wa Simba Haruna Niyonzima ameanza mazoezi na wenzake baada ya kuwa nje kwa muda mrefu akiuguza majeraha. Niyonzima alikwenda india kwa ajili ya matibabu ambapo ilielezwa ,,,,,
angefanyiwa upasuaji mdogo lakini jambo zuri ni kwamba alitibiwa bila kufanyiwa upasuaji.
Niyonzima anaamini baada ya muda mfupi atarudi uwanjani baada ya kumaliza program za mwalimu.
“Siwezi kuja mazoezini kabla sijawa vizuri, lakini siwezi kuesema nipo vizuri kwa 100% watau wanachotakiwa kujua, mtu ukitoka kwenye maumivu huwezi kuja kujiunga na timu moja kwa moja lakini ninachoshukuru naona kama napiga hatua kwa sababu siku za nyuma nilikuwa nyumbani lakini sasa nimeanza kuungana na timu.”
“Kwa sasa najisikia nafuu na nimeanza kupewa ratiba na mwalimu naamini mambo yatakuwa mazuri. Kuna ‘recover’ za ina mbili kuna ya daktari na mwalimu, ya daktari tayari nimeshafanya sasa hivi nafanya ya mwalimu kwa hiyo ikiisha najiunga na timu.”
“Nimemi-miss kucheza kwa sababu muda mrefu sijacheza na watu wanajua mpira ni kazi yangu lakini siwezi kuchukua uamuzi nikasema nacheza, natakiwa kwenda na ratiba ya timu, daktari na mwalimu lakini sasa hivi nipo kwenye ratiba ya mwalimu, muda si mrefu nitarudi uwanjani.”
Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.