Header Ads

ad

Fatma Karume achukua mikoba ya Lissu TLS

Leo April 14, 2018 umefanyika uchaguzi katika chama cha Mawakili wa Tanganyika ambapo Wakili maarufu
nchini Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais mpya  wa Chama hicho kwa kupata kura 820.
Nafasi hiyo ya Urais  ilikuwa ikigombewa na Mawakili wengine watatu ambao ni, Simba Ngwilimi ambaye amepata 363, Musa Mwapongo kura 12 na Godfrey Wasonga kura 6.
Katika uchaguzi huo, Dkt Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa TLS kwa kupata kura 1170. Fatma anachukua nafasi ya Tundu Lissu ambaye amemaliza muda wake.
Kwa upande wa Zanzibar Wakili Omar Said Shaaban amechaguliwa kuwa Rais Mpya wa chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS)
Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.