Header Ads

ad

Kwanini ujauzito hutungwa kipindi cha kunyonyesha?

Msomaji (jina nalihifadhi) alinitumia ujumbe wa maneno akisema; alijigundua ana ujauzito wakati mtoto wake akiwa na umri wa miezi mitano na huku akiwa bado ananyonya.

Jambo hili lilimstua kwasababu anavyofahamu hawezi kupata ujauzito kwakuwa ananyonyesha.

Ni kweli wanawake wengi wanadhani kuwa hawawezi kupata ujauzito kipindi wanachonyonyesha hasa kutokana na kutopata hedhi au kupata hedhi kidogo katika miezi ya awali tangu wajifungue.

Kitabibu ni sahihi, kunyonyesha ni mojawapo ya njia ya asili ya uzazi wa mpango ambayo watu wenye imani za kidini wanakubali kuitumia.
Ieleweke kuwa uwezo wa kupata mimba unakuwa mdogo kwa mwanamke anapokuwa ananyonyesha mara kwa mara ila siyo sahihi kusema njia hii inakuzuia kupata ujauzito kabisa.

Njia hii inafanya kazi zaidi na kuweza kuzuia mimba kwa asilimia 98 endapo tu mtoto anapokuwa na umri wa miezi sita na ana tumia maziwa ya mama tu, ambayo anayanyonya mara kwa mara, mchana na usiku.

Pia, kama mama huyo atakuwa bado hajapata hedhi ya kila mwezi tangu alipojifungua.
Je ni kwa vipi kunyonyesha ni njia mojawapo ya kuzuia ujauzito. Wakati mwanamke ananyonyesha, huwa inazuia au kuchelewesha mzunguko wa hedhi kutokea.
Mwanamke anaponyonyesha husababisha kusisimuliwa kwa kichochezi (hormon) kijulikanacho kitabibu kama prolactin au milk hormon.

Kiwango cha kichochezi hiki kinapokuwa kipo juu mwilini, huzuia viwango vya vichochezi vinavyochea upevushwaji wa kijiyai cha kike (ovulation).

Na hii ndiyo sababu hata mizunguko ya hedhi ya wanawake wanaonyonyesha kutoonekana katika miezi ya awali baada ya kujifungua au anaweza kuwa na mzunguko unao badilika badilika.

Kadiri miezi inavyosogea baada ya kujifungua, kiwango cha kichochezi cha prolactin hupungua, ndiyo maana wengi wanaonyenyesha huwa hawapati ujauzito katika miezi mitatu ya awali.

Kwa mwanamke ambaye ametoka kujifungua na ananyonyesha kabla ya kuanza tena kupata tena mzunguko wake wa hedhi, hutanguliwa kwanza na kuanza kupevushwa kwa kijiyai cha kike.

Wanawake wengi huwa hawajui kama kijiyai cha kike kimepevushwa na kipo tayari kuungana na mbegu ya kiume ili kutunga mimba mpaka tu pale zinapopita wiki mbili na kupata hedhi yake.

Kwa kawaida, kijiyai cha kike kisipopevushwa na mbegu ya kiume baada ya kushiriki tendo la ndoa, ndipo hedhi hutokea.
Wanawake wanaopata ujauzito kipindi cha unyonyeshaji ni wale ambao watoto wao wanaacha kunyonya mapema au watoto wao wanalala sana na kutonyonya vizuri usiku.
Hii ni kwasababu kile kiwango cha kichochezi cha pralactin kinapungua, hivyo wanaweza kupata mimba ndani ya miezi mitatu hadi tisa tangu alipojifungua.

Wanawake wengine wanaopata ujauzito kipindi hiki ni pamoja na wale ambao wamewaachisha watoto wao kunyonya na kuwapa maziwa ya chupa.
Pia, wale ambao wanawanyonyesha huku wanawapa maziwa ya chupa kipindi cha miezi ya awali baada ya kujifungua, nao wapo katika hatari yakupata mimba kipindi hiki cha unyonyeshaji.

Vile vile watakapoaanza kuwapa watoto wao vyakula vya kulikiza (weaning), huwa ni baada ya kufikisha miezi sita nao wanakuwa katika hatari ya kushika ujauzito wakiwa wananyonyesha.

Hivyo, tunaona kuwa mimba inaweza kutungwa kipindi cha unyonyeshaji.
Ni vizuri kama huitaji kupata ujauzito kipindi hiki tumia njia nyigine za uzazi wa mpango mapema pale utakapokuwa tayari umeanza tena kujamiana bila kinga na mwenza wako.
Ch
Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.