Header Ads

ad

HABARI MPYA TOKA SERIKALINI KWA WALIOKUWA WAMEONDOLEWA KAZINI

Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika imetoa tamko la kuwarejesha kazini wafanyakazi waliokuwa wameondolewa kazini wakati wa uhakiki wa vyeti kutokana na kukosa sifa ya cheti cha kufaulu mtihani wa kidato cha nne.


Akizungumza Bungeni Leo, Waziri Mkuchika amesema kuwa watumishi ambao walikuwa wameajiriwa ajira za kudumu, za mkataba au za muda kabla ya Mei @0, 2004 wanapaswa kurejeshwa kazini, kulipwa mishahara yao kwa muda wote waliokuwa wameondolewa pamoja na kuendelea na kazi mpaka pale watakapostaaafu kwa mujibu wa sheria.

“Watumishi wote ambao walikuwa na ajira za kudumu, za mikataba au za muda ambao walikuwa kazini kabla ya Mei 20, 2004 ulipoanza kutumika waraka wa utumishi wa mwaka 2004, warejeshwe kazini mara moja, walipwe mishahara yao kwa kipindi chote ambacho walikuwa wameondolewa kazini na waendelee na ajira zao hadi watakapostaafu kwa umri kila mmoja.” amesema Waziri George Mkuchika.

Lisome hapa tamko lililotolewa bungeni na Wizara ya Utumiishi na Utawala Bora.




Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.