Header Ads

ad

Simba imeendelea kukusanya point zake VPL

Wekundu wa Msimbazi Simba SC Jumatatu ya April 9 2018 walishuka katika uwanja Jamhuri Morogoro kucheza na wenyeji wao Mtibwa Sugar, huo ukiwa ni mchezo wao wa 22 wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2017/2o18 kwa Simbaambayo kwa ...
sasa imesalia katika mashindano hayo pekee.
Timu za Dar es Salaam ambazo mara nyingi zimekuwa zikihangaika kupata matokeo katika viwanja vya mikoani kwa madai ya viwanja vibovu, imekuwa tofauti kwa Simba ambayo imefanikiwa kuondoka na point tatu katika uwanja huo kufuatia kupata ushindi wa goli 1-0 lililofungwa na Emmanuel Okwi dakika ya 24.
Ushindi huo sasa unaifanya Simba kufikisha jumla ya point 52 na kuendelea kusalia kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu, wakifuatiwa na wapinzani wao Yanga waliyopo nafasi ya pili kwa kuwa na jumla ya point 46 ila wapo nyuma mchezo mmoja nyuma ya  Simba, wakati Mtibwa Sugar imeendelea kusalia nafasi ya sita kwa kuwa na jumla ya point 30.
Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.