Header Ads

ad

Wazanzibar wakumbuka kifo cha Karume.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na mamlaka husika itatafakari namna bora zaidi ya kukusanywa kwa...
Kumbukumbu muhimu za Kiongozi wa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar  Marehemu Mzee Abeid Aman Karume  ili ziwe kielelezo cha Taaluma kwa Kizazi cha sasa.

Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo baada ya kuyapokea Matembezi  Maalum ya Vijana  400 wa Chama cha Mapinduzi ya kumuenzi Mzee Abeid Aman Karume  yaliyoanzia Kijiji alichozaliwa cha Mwera Kiongoni  na kumalizia katika Viwanja vya Afisi Kuu ya CCM  Kisiwanduzi Mjini Zanzibar.

Amesema Kumbukumbu hizo ndio njia pekee ya kuendelea kumuenzi Kiongozi huyo  kwa kufuata fikra na mawazo aliyowaachia  Wananchi wa Zanzibar wakielewa kwamba yeye ndie aliyeongoza mapambano dhidi ya Wakoloni na hatimae kupatikana kwa Ukombozi wa Visiwa vya Zanzibar.
Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.