Header Ads

ad

Mashabiki Liverpool waliamsha ‘dude’ huko Ulaya, waishambulia UEFA mitandaoni ikidaiwa kisa hiki..

Mashabiki wa Liverpool kweli wamepagawa na timu yao kuingia fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Ndiyo maana siku walipoitoa AS Roma kwa jumla ya mabao 7-6 wakafunga baa za Roma, walikunywa hadi asubuhi, kelele kila kona za mitaa ya Roma wakijielekeza kwenye fainali itakayopigwa Mei 26 kwenye mji wa Kiev, Ukraine.

Sasa sikia hii. Waandaaji wa fainali hiyo, Shirikisho la Soka Ulaya, (Uefa), limewaambia kuwa wasijipe matumaini kwamba mashabiki wake wote wataingia kwenye Uwanja wa NSC Olimpiyskiy siku hiyo ya fainali, hilo halipo.

Uefa limewaambia kuwa kama vipi wajichuje kwani wametengewa tiketi 17,000 tu kwa watakaobahatika kuingia uwanjani. Juzi waliofika Roma kuwashangilia Liverpool walikuwa mashabiki wasiopungua 5,000.

Baada ya kupata taarifa hizo kwamba wamewekewa nafasi 16,626 kila mmoja alifyonya na kusema lake wakiitaka Ueafa kuwaongezea tiketi kwa kuwa wako wengi na 16,626 haziwatoshi.

Uwanja utakaochezewa fainali una uwezo wa kuzoa mashabiki 63,000.
Hata hivyo, karibu robo ya tiketi inakaribia kumalizika na mashabiki wameingia kwenye mitandao ya kijamii wakiishutumu Uefa kwa kuwabania.

Uefa katika taarifa yake, ilisema kuwa kila klabu imepewa tiketi 17,000 huku Liverpool ikisema kuwa kati ya tiketi hizo, 250 lazima waopewe wachezaji, kwa ajili ya familia zao na kamati za ufundi na nfdiyo maana zimebaki 16,626, huku ikielezwa kuwa wanaweza kuuza idadi hiyo hata zaidi ya mara 10.

Inaelezwa kwamba huko Anfield mipango inafanywa kuwaona Uefa kwa ajili ya kuongeza idadi ya tiketi kwa watakaosafiri kwenda kwenye fainali huko Kiev.

Mpaka sasa tiketi 6,700 zimeshauzwa kupitia mtandao, na kwamba Uefa imesema asilimia 65 ya watu 63,000, zitakuwa nafasi za mashabiki na kwamba mgawanyo huo ni sawa na ilivyokuwa msimu uliopita.

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.