Header Ads

ad

Ni Rea Madrid au Liverpool?? Nani Kuibuka Mshindi??

Leo tunaungazia mchezo wa fainali ya Uefa Champions League, inayotaraji kupigwa kesho Jumamosi ya Mei 26, 2018 pale Kiev.

Mengi yamekuwa yakizungumzwa baina ya timu hizi mbili zinazokutana kesho, Real Madrid na Liverpool mashabiki wamekuwa wakiangazia safu zote za  timu hizi kuanzia ushambualiaji, ulinzi na eneo la kiungo.

Lakini hapa nakuletea makala ambayo nitaangazia maeneo mawili ya ulinzi na ushambuliaji kwa kwa kila timu, hapa ni kwa takwimu zao za michezo iliyopita.

Real Madrid katika michezo yao 12, ya UCL msimu huu wamefanikiwa kupata Clean sheets 3 tu, hii ina maana katika michezo yao 9 waliruhusu mabao kufungwa.

Tofauti ya msimu wa 2016/17 waliruhusu mabao 17, msimu huu wamesharuhusu mabao 15, katika UCL na rekodi zinaonesha kuanzia msimu wa 2003/4 hakuna timu ambayo ilifika fainali ikiwa imeruhusu kuanzia idadi ya mabao 15.

Hapo unaweza kuona ni namna gani hali ya safu ya ulinzi ya Los Blancos ilivyo kwa sasa kabla ya kuelekea katika mchezo wa fainali.

Liverpool hadi sasa wameruhusu mabao 13, katika lango lao mabao 6 yakiwa katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya AS Roma, hii ikiwa ni mabao 2 nyuma ya Real Madrid huku Liverpool wakiwa na clean sheets 6 ikiwa ni 3 zaidi ya Real Madrid.

Liverpool wameonekana kuwa na tatizo la kupoteza umakini hasa kuanzia dakika za 60, za mchezo rekodi zikionesha katika michezo 5 iliyopita ya UCL kwa dakika 15, za mwanzo waliongoza waliongoza kwa mabao 11-4 ili hali dakika 15 za mwisho waliongozwa kwa mabao 6-1 katika michezo hiyo.

Katika safu za ushambuliaji;

Kwa takribani miaka kadhaa sasa Real Madrid imeonekana kuwa na safu kali ya ushambuliaji, msimu wa mwaka 2014/15 Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Gareth Bale walifunga jumla ya mabao 28, wakivunja rekodi ya mabao 27, iliyowekwa na MSN(Messi, Suarez na Neynar Jr) msimu wa mwaka 2013/14.

Lakini hali imekuwa tofauti kwa msimu tayari Liverpool wametambulisha utatu wao kama ni safu kali sana ya ushambuliaji, wakifunga jumla ya mabao 30, hadi sasa  na kufanikiwa kuvunja rekodi ya mabao 28, iliyowekwa na BBC.

Sadio Mane, Mohammed Salah na Roberto Firminho kila mmoja amefunga mabao 10, hadi sasa kunako michuano ya UCL msimu huu.

Cristiano Ronaldo amefunga mabao 15, hadi sasa, ikiwa ni mabao 5 zaidi ya safu nzima ya ushambuliaji ya Liverpool, lakini pia akihitaji mabao mawili kufikia rekodi yake ya kufunga mabao 17, katika msimu wa mwaka 2014/15.

Tupe utabiri wako wewe. Unadhani nani ataibuka mshindi kesho.?

No comments:

Theme images by merrymoonmary. Powered by Blogger.